Je wajua historia ya tajiri wa pili duniani Warren Buffet?
Je wajua historia ya Tajiri wa pili Duniani Warren Buffet
Je wajua historia ya tajiri wa pili duniani Warren Buffet? Yeye anamiliki zaidi ya dola za kimarekani bilioni 50 na ameshachangia zaidi ya billion 30. Haya ndio baadhi ya mambo yake muhimu kuzingatia:
Alinunua shea za kwanza akiwa na miaka 11 tu. Sasa anajuta kuwa alichelewa kununua shea
Alinunua kashamba kadogo akiwa na miaka 14 tu kwa fedha alizodunduliza kwa kusambaza magazeti
Bado anaishi katika kijumba chake kisicho na fensi cha vyumba vitatu mpaka sasa iliyopo katika mji mdogo wa Omaha. Nyumba hiyo aliinunua miaka 50 iliyopita wakati anaoa. Anadai nyumba hiyo ina kila kitu anachohitaji kwa hiyo haitaji nyumba zaidi
Anaendesha gari lake mwenyewe na hana dereva wala mlinzi
Hasafiri kamwe na ndege binafsi japo anamiliki kampuni ya ndege kubwa kuliko zote duniani
Kampuni yake ya Berkshire inamiliki makampuni 63. Huandika barua moja kila mwaka kwa wakurugenzi wa hizo kampuni akiwapo mwelekeo tu. Hafanyi mikutano wala kuwaita wakurugenzi mara kwa mara.
Amewapa wakurugenzi wake masharti mawili tu
Usipoteze pesa za wenye hisa
Usisahau sharti la kwanza
Hajichanganyi sana na jamii ya matajiri, maisha yake baada ya kuoa ni pop corn na kuangalia TV tu
Warren Buffet habebi simu wala hana kompyuta kwenye dawati lake
Billgates (Tajiri wa pili dunuani baada ya …wa Mexico ) alikutana nae kwa mara ya kwanza miaka 5 iliyopita. Billgates alidhani hana mambo yanayolandana na Warren Buffet, kwa hiyo alipanga kuonana nae kwa nusu saa tu lakini walipokutana walilonga kwa masaa zaidi ya kumi (10) na tangu hapo Billgates akawa mfuasi wa karibu wa Waren Buffet
Ushauri wake kwa vijana ni huu
Kaa mbali na kadi za kusugua au mtandaoni yaani credit cards (Yeye anaziita mikopo ya benki) na uwekeze kwa wewe mwenyewe
Pesa hazikumuumba mtu, bali mtu ndie aliyeziumba pesa
Ishi maisha yako rahisi na halisi kama ulivyo
Usitende yale wengine wayasemayo, bali wasikilize na wewe fanya unayojisikia ni mazuri
Usihatamie vitu vyenye majina, vaa vitu unavyoona vinakupa raha
Usitumie vibaya pesa zako, tumia tu pale kuna uhitaji
Baada ya yote, hayo ni maisha yako kwanini uwape wengine wayaongoze maisha yako?
Maisha mazuri sio lazima yawepo katika vitu vizuri. Maisha rahisi na halisi ndio masiha mazuri
Today, there have been 6 visitors (13 hits) on this page!